1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Jumuiya ya Ulaya yagawanyika kuhusu kuondoa vikwazo vya silaha dhidi ya China.

23 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFUJ

Mgawanyiko umetokea katika mkutano wa jumuiya ya Ulaya juu ya kuondoa vikwazo vya silaha dhidi ya China. Rais wa Ufaransa Jacques Chirac ametaka kulipa uzito wa chini suala la wasi wasi wa kuiondolea vikwazo vya silaha China, akiliambia gazeti moja la Japan kuwa hatua hiyo haina maana kuwa jumuiya ya Ulaya itaanza mara moja kuuza silaha kwa China. Mataifa mengine wanachama wameeleza wasi wasi wao kuhusiana na China kupitisha sheria ikiidhinisha matumizi ya kijeshi dhidi ya Taiwan iwapo nchi hiyo itajitangazia uhuru. Mataifa wanachama wa jumuiya ya Ulaya wanatarajiwa kuchelewesha kuondolewa kwa vikwazo hivyo hasa kutokana na upinzani dhidi ya hatua hiyo kutoka Marekani. Baraza la Kongress la Marekani limetishia kuchukua hatua dhidi ya mataifa wanachama wa umoja wa Ulaya iwapo vikwazo hivyo vitaondolewa.