1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS Croatia bado haijafaulu kujumulishwa katika umoja wa Ulaya

8 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF5W

Halmashauri ya jumuiya ya Ulaya imesema kwamba Croatia haijafanya juhudi za kutosha kuyawezesha mazungumzo ya kutaka kuwa mwanachama wa jumuiya hiyo kuanza.

Kwa mujibu wa ripoti ya umoja wa mataifa, iliyotayarishwa na muongoza mashtaka mkuu wa umoja huo, Carla del Ponte, serikali ya Zagreb haishirikiani na umoja huo kumtafuta mtuhumiwa mkuu wa uhalifu wa kivita nchini humo.

Kamishna anayeshughulikia upanuzi wa umoja wa Ulaya, Olli Rehn, amesema Croatia imefaulu katika sehemu chache, lakini imeshindwa kushirikiana kikamilifu na tume inayochunguza visa vya uhalifu wa kivita mjini The Hague. Del Ponte anataka jenerali wa zamani, Ante Gotovina, na watuhumiwa wengine wafikishwe mbele ya tume hiyo kabla kusema taifa hilo linashirikiana kwa dhati katika kesi hiyo.

Habari zaidi kutoka Brussels zinasema mawaziri kutoka mataifa wanachama wa jumuiya ya kujihami ya kambi ya magharibi ya NATO watakutana hapo kesho mjini Brussels kujadili njia za kuwasaidia walinda usalama wa umoja wa Afrika walio katika eneo la Darfur nchini Sudan.