1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: China yalalama iondolewe vikwazo vya silaha.

23 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFUP

Viongozi wa Umoja wa nchi za Ulaya wako Brussels Ubelgiji katika mkutano wa kutafuta mikakati ya kudumisha hali ya uchumi ya umoja huo na swala la litakalo jadiliwa kwa kina ni swala la kulegeza masharti ya soko la ndani.

Kuna ishara kuwa huenda kukazuka upinzani katika mashauriano hayo juu ya utendaji kazi wa mswada huo. Ujerumani na Ufaransa zinapinga mswada huo kwa sasa, lakini dalili zaonyesha kuwa mabadiliko yatapatikana.

Wakati huo huo China imeutaka Umoja wa Ulaya kuendelea na mpango wa kuiondolea vikwazo vya silaha vya miaka15 iliyopita.

Jopo la wanachama 25 wa Umoja wa Ulaya huenda likachelewesha uamuzi wa kuiondolea China vikwazo hivyo kufuatia uamuzi wa bunge la Beijing wa kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya Taiwan.

Marekani imeutaka Umoja huo kutoiondolea China vikwazo hivyo hatua ambayo msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China amelalamika kuwa huo ni ubaguzi wa kisiasa.

Viongozi wa Umoja wa nchi za Ulaya utalizungumzia swala hilo la kuiondolea China vikwazo vya silaha katika mkutano wao wa siku mbili mjini Brussels.