1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Blair ameshauri mageuzi katika Umoja wa Ulaya

24 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF0m

Waziri Mkuu wa Uingereza,Tony Blair akilihotubia bunge la Umoja wa Ulaya mjini Brussels amesema,Umoja huo unakabiliwa na „mzozo katika uongozi wa kisiasa.“ Akaongezea kuwa Umoja wa Ulaya unapaswa kufanya mageuzi ili upate kurejesha imani ya umma.Blair,alieleza mawazo yake kuhusu wadhifa wa urais wa Umoja huo unaozunguka na utakaopokewa na Uingereza tarehe mosi Julai.Ametoa muito pia wa kufanywa mageuzi makubwa.Aliwashutumu wale wanaodai kuwa Uingereza inajaribu kuufanya Umoja huo kama eneo la biashara huru tu,akiongezea kuwa yeye anaunga mkono kuwa na Ulaya iliyo jamii ya kisasa.Waziri mkuu Blair ametamka hayo baada ya viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya,katika mkutano wao wiki iliyopita,kushindwa kukubaliana kuhusu bajeti ya Umoja huo.Wengi wamemlaumu Blair kwamba hakuwa tayari kuafikiana.