1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brusels.Umoja wa Uláya kuweka mkakati wa pamoja wa kuzuia wimbi la wakimbizi.

26 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CD8h

Nchi kadhaa wanachama wa Umoja wa Ulaya zimeutaka umoja huo kuwa na mkakati wa aina moja kupambana na wimbi la wakimbizi kutoka eneo la bahari ya kati.

Katika risala aliyopelekewa mwenyekiti wa sasa wa Umaja wa Ulaya Finland, viongozi wa mataifa manane zikiwemo Ufaransa, Italy, Hispania na Ureno wameonya suali hili kuwa linastahiki kushughulikiwa na nchi zote wanachama.

Maefu ya waafrika wameyatia maisha yao hatarini na kuingia katika visiwa vya Canary vya Hispania katika bahari ya kati.

Wakati huo huo ofisi kuu ya takwimu nchini Ujerumani imetangaza kupungua idadi ya watu wanaoomba ukimbizi nchini Ujerumani kwa mwaka 2005.

Ofisi hiyo imesema watu laki mbili na elfu tisa wamejiandikisha kuomba ukimbizi mwaka jana, idadi hiyo ni ndogo kwa asilimia kumi ikilinganishwa na mwaka juzi.