1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brazil yaomboleza vifo vya watu 61 katika ajali ya ndege

10 Agosti 2024

Rais Inacio Lula da Silva wa Brazil ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa, kufuatia ajali ya ndege katika jimbo la Sao Paulo iliyouwa watu wote 61 waliokuwemo.

https://p.dw.com/p/4jKD2
Brazil
Rais wa Brazil Inacio Lula da Silva Picha: Ricardo Stuckert/AFP

Ndege chapa ATR 72-500 inayomilikiwa na kampuni ya Voepass ilianguka jioni ya jana katika mji wa Vinhedo, wakati ikitokea jimbo la kusini la Parana kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sao Paulo. 

Juhudi za kuipata na kuitambua miili zilikuwa zinaendelea hadi alfajiri ya leo. Mamlaka ya ajali za anga ya Brazil, CENIPA, imetangaza kuanza uchunguzi wa ajali hiyo mara moja.

Ajali ya ndege yauwa watu 61 Brazil

Kampuni ya ATR ambayo ndiyo iliyoiunda ndege hiyo, imesema wataalamu wake wanashirikiana na mamlaka za uchunguzi. Takwimu zinaonesha kuwa ajali 108 za ndege zimetokea mwaka huu peke yake nchini Brazil.