1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiBrazil

Ajali ya ndege yauwa watu 61 Brazil

10 Agosti 2024

Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa, kufuatia ajali ya ndege iliyouwa watu wote 61 waliokuwemo katika jimbo la Sao Paulo.

https://p.dw.com/p/4jJbl
Mto ukiwaka kufuatia ajali ya ndege mjini Vinhedo, Sao Paulo.
Mto ukiwaka kufuatia ajali ya ndege mjini Vinhedo, Sao Paulo. Picha: Felipe Magalhaes Filho/AP/picture alliance

Ndege chapa ATR 72-500 inayomilikiwa na kampuni ya Voepass ilianguka jioni ya jana katika mji wa Vinhedo, wakati ikitokea jimbo la kusini la Parana kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sao Paulo.

Juhudi za kuipata na kuitambua miili zilikuwa zinaendelea hadi alfajiri ya leo.

Soma zaidi: SAO PAULO:Brazil yaomboleza,rambirambi kutoka kote ulimwenguni

Mamlaka ya ajali za anga ya Brazil, CENIPA, imetangaza kuanza uchunguzi wa ajali hiyo mara moja.

Kampuni ya ATR ambayo ndiyo iliyoiunda ndege hiyo, imesema wataalamu wake wanashirikiana na mamlaka za uchunguzi.

Takwimu zinaonesha kuwa ajali 108 za ndege zimetokea mwaka huu peke yake nchini Brazil.