1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRAZAVILLE: Ugonjwa hatari wa Ebola walipuka-

25 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CFy6
Watu wasiopungua kumi na wanane wamefariki dunia tangu mwezi October uliopita, kutokana na ugonjwa hatari wa Ebola, uliojitokeza katika jimbo la Mbomo, kaskazini magharibi mwa Congo-Brazaville. Kwa mujibu wa jarida la maswali ya afya la serikali ya Jamuhuri ya Congo, watu wa kwanza waliogunduliwa kua na ugonjwa huo, walipatikana katika kijiji cha Mbanza, na katika kijiji cha Oloba, mpakani na Gabon. Wizara ya afya imesema imewatuma wataalamu wake katika maeneo hayo, na kuonya dhidi ya uwezekano wa ugonjwa huo kusambaa katika maeneo mengine zaidi, kutokana na watu kutotekeleza ushauri wa kujilinda, wanaopewa na maafisa wa wizara ya afya. Mpaka sasa hakuna dawa wala kinga ya ugonjwa huo-