1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BOUAKE: Makubaliano kusalimisha silaha nchini Ivory Coast

17 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFME

Serikali ya Ivory Coast na makamanda wa majeshi ya waasi wamekubaliana kwa masharti fulani kupanga tarehe ya kusalimisha silaha na kuhamisha silaha kubwa kubwa kutoka mipaka ya maeneo ya mapambano, kuanzia tarehe 21 mwezi huu.Katika hati ya pamoja,pande hizo mbili pia zimesema zitachunguza pendekezo lililotolewa na halmashauri maalum kuwa silaha zisalimishwe kati ya Mei 14 na Julai 31.Majadiliano ya kusalimisha silaha yaliofanywa mjini Bouake nchini Ivory Coast,ni sehemu muhimu ya makubaliano ya amani yaliopatikana wiki iliyopita nchini Afrika ya Kusini.Pande zote mbili zilikubaliana kusitisha mapigano na kuitisha uchaguzi wa rais mwezi wa Oktoba.Vita vilichomoza nchini Ivory Coast mwaka 2002,baada ya waasi kujaribu kumpindua rais Laurent Gbagbo.Kiasi ya wanajeshi 10,000 wa Umoja wa Mataifa na Ufaransa hivi sasa wanalinda amani nchini Ivory Coast katika eneo ambako silaha zimepigwa marufuku.