1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Borell: Uamunifu kati ya Umoja wa Ulaya na China umepotea

13 Oktoba 2023

Borell aidha amesisitiza kwamba uwiano unakosekana kati ya Umoja wa Ulaya na China upande wa viwango na ubora na hali hii inaathiri sekta ambazo wanapata faida.

https://p.dw.com/p/4XUcK
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borell
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep BorellPicha: Philipp von Ditfurth/dpa/picture alliance

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borell ametahadharisha kwamba uaminifu wa pamoja kati ya umoja huo na China umepotea. Akizungumza hivi leo katika chuo kikuu cha Peking mjini Beijing, Borell amesema wana wajibu wa kuujenga upya uaminifu huo kwa kuwa hautarudi kwa njia ya muujiza.

Borell aidha amesisitiza kwamba  uwiano unakosekana kati ya Umoja wa Ulaya na China upande wa viwango na ubora na hali hii inaathiri sekta ambazo wanapata faida.

Borell aliwasili nchini China jana Alhamisi katika ziara inayolenga kupunguza misuguano kati ya Umoja wa Ulaya na China na pia kuandaa mkutano wa kilele baina ya pande hizo mbili baadaye mwaka huu.

Ziara ya Borell inayoendelea hadi kesho Jumamosi ilianzia Shanghai ambako alikutana na kampuni za Ulaya kujadili changamoto za kiuchumi na kibiashara.