1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bonn. Rais wa Ujerumani afanya juhudi za kuisaidia Afrika.

6 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CELG

Rais wa Ujerumani Horst Köhler amefungua mkutano wa siku mbili hapa mjini Bonn, ambao unaangalia kuhusu misaada katika bara la Afrika.

Mkutano huo ni sehemu ya juhudi za rais Köhler zinazojulikana kama ushirikiano na Afrika.

Anataka kuanzisha majadiliano kati ya nchi zenye utajiri wa viwanda na mataifa ya Afrika.

Mkutano huo , ambao unamalizika leo Jumapili , umewaleta pamoja wanasiasa , wasomi na wafanyabiashara ambao wanapendelea kutafuta mikakati mipya ya kutoa misaada ya maendeleo kwa bara la Afrika. Siku ya kwanza ya mkutano huo ilitawaliwa na kundi la Waethiopia wapatao 400 waliofanya maandamano dhidi ya serikali ya waziri mkuu wao Meles Zenawi.

Siku nne za machafuko nchini ethiopia zimesababisha watu zaidi ya 40 kupoteza maisha. Vyama vya upinzani vinasema kuwa chama tawala kimefanya njama za wizi wa kura katika uchaguzi wa bunge mnamo May mwaka huu.