1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BONN: Mkutano juu ya Afrika waendelea mjini Bonn

7 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEKu

Mkutano unaojadili maswala ya Afrika unaendelea hapa mjini Bonn, Ujerumani. Rais wa Ujerumani, Horst Köhler, ameundaa mkutano huo unaolenga kuboresha utoaji wa misaada ya maendeleo barani Afrika. Mkutano huo unalenga kuanzisha mdahalo kati ya mataifa yaliyoendelea kiviwanda duniani na bara la Afrika.

Mkutano huo umewaleta pamoja wanasiasa, wasomi na viongozi wa kibishara kuzunguzia juu ya mikakati mipya ya maendeleo barani Afrika.