1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BONN: Makao mapya ya mashirika ya Umoja wa Mataifa

11 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG8T

Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan wamefungua makao mapya ya mashirika ya Umoja wa Mataifa mjini Bonn,ambao hapo zamani ulikuwa mji mkuu wa Ujerumani.Makao hayo yapo katika jengo ambalo hapo awali lilitumiwa na wabunge.Serikali ya Ujerumani imetumia Euro milioni 56 kulifanyia ukarabati jengo hilo la ghorofa na sasa Umoja wa Mataifa unaruhusiwa kutumia bure jengo hilo.Mashirika 12 ya Umoja huo ambayo hapo zamani yalikuwa sehemu mbali mbali mjini Bonn,sasa yatakuwa katika jengo moja.Katika sherehe ya kuyafungua makao hayo,Kofi Annan aliwashukuru wenyeji wake kwa mchango unaotolewa kwa kazi za Umoja wa Mataifa.