1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bomoa bomoa inaendelea Zimbabwe

10 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEvh

Harare:

Zoezi la bomoa bomoa nchini Zimbabwe, ambalo limewafanya watu elfu kadhaa kutokuwa na mahali pa kuishi, sasa litatekelezwa katika sehemu zenye nyumba za fahari mjini Harare. Majengo ambayo hayakuidhinishwa kama vile nyumba nyongeza za Watumishi na magereji yatavunjwa. Redio ya taifa leo imemnukulu Mkuu wa Polisi, Loveless Rupere, akisema kuwa wakazi wa vitongoji vya Harare wanapaswa kuvunja majengo yasiyoidhinishwa na waweke hati zao tayari za kuwaonyesha polisi wakati watakapoanza zoezi la bomoa bomoa kesho Jumatatu. Serikali ya Zimbabwe imeanza operesheni bomoa bomoa Mei 19 kwa kuvunja majengo yasiyoidhinishwa katika zile sehemu za madongo poromoka ili kupunguza ujambazi. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, watu 200,000 hawana makazi ingawaje upinzani unasema kuwa jumla yao ni millioni moja na nusu.