1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bolsonaro kukata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama

1 Julai 2023

Rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro, ameapa kupambana kwa kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama moja ya nchi hiyo ya kumpiga marufuku kuwania nafasi yoyote ya umma katika kipindi cha miaka minane.

https://p.dw.com/p/4TIZ5
USA, Florida | Jair Bolsonaro
Picha: Paul Hennessy/AA/picture alliance

Uamuazi huo uliotolewa jana unatokana na matamshi ya Bolsonaro ya mwaka 2022 alipoukosoa mfumo wa upigaji kura wa nchi hiyo bila kutoa ushahidi.

Mwanasiasa huyo wa mrengo wa kulia amewaambia waandishi habari kwamba uamuzi wa mahakama ni "usaliti" na anajitayarisha kukata rufaa kwenye mahakama kuu.

Hukumu hiyo ya mahakama inaamanisha Bolsonaro hataruhusiwa kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi wa mwaka 2026.

Alipelekwa mahakamani na tume ya uchaguzi ya nchi hiyo kwa kutoa madai bila ushahidi kwamba, mfumo wa upigaji kura kwa njia ya elektroniki unaotumika nchini Brazil tangu mwaka 1996 umevuruga uwazi kwenye uchaguzi.