1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BOCHUM:Schroeder ataka Umoja wa Ulaya uwe na sauti moja

17 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CG0J
Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani ametumia hotuba yake katika mkutano mkuu wa chama chake cha Social Demokrat kutaja baadhi ya masuala muhimu ya sera ya mambo ya nje ya Ujerumani. Schroeder amewaambia wajumbe wa chama cha SPD wanaokutana huko Bochum kwamba Umoja wa Ulaya una dhima kubwa ya kutimiza katika dimplomasia ya kimataifa.Amesema kwamba baada ya Umoja wa Ulaya kuzikaribisha nchi 10 wanachama wapya hapo mwakani umoja huo lazima uwe na sauti moja kufanya kila iwezalo kuzima migogoro ya kijeshi inayozidi kuongezeka.Lengo kuu la mkutano huo ni kuandaa orodha ya wagombea kwa ajili ya uchaguzi wa mwezi wa Juni wa umoja wa Ulaya.Mbunge wa hivi sasa wa bunge la Umoja wa Ulaya Martin Schulz amechaguliwa kuwa miongoni mwa wagombea wakuu wa chama cha SPD.