1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bobi Wine ahimiza jamii ya kimataifa kumuunga mkono

5 Februari 2021

Mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine ameihimiza jaumuiya ya kimataifa kuunga mkono juhudi zake za kupinga matokeo ya uchaguzi wa nchi hiyo unaodaiwa kukumbwa na kasoro.

https://p.dw.com/p/3oxGc
Uganda | Opposition | Bobi Wine
Picha: Nicholas Bamulanzeki/AP Photo/picture alliance

Bobi Wine ataka jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua kali dhidi ya serikali ya rais Yoweri Museveni.

Akizungumza kupitia njia ya video kutoka nyumbani kwake nje kidogo ya mji mkuu, Kampala ambapo amesema bado yuko chini ya kifungo cha nyumbani, Bobi Wine amesema kuwa Museveni kama viongozi wengine madikteta hatishiki kwa maneno.

Bobi Wine ambaye majina yake halisi ni Robert Kyagulanyi, amewaambia wanahabari ana matumaini kwamba mataifa ya duniani yatasimama na watu wa Uganda.

Akizungumzia kuhusu shtuma za kimataifa dhidi ya matokeo ya uchaguzi huo, mwanasiasa huyo wa upinzani ameongeza kuwa wanatarajia hatua zaidi kufuatia shtuma hizo.