1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Antony Blinken akutana na waziri wa mambo ya nje Ethiopia

15 Machi 2023

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken amekutana leo na mwenzake wa Addis Ababa Demeke Mekonnen.

https://p.dw.com/p/4OhWy
Äthiopien | Ankunft Antony Blinken in Addis Abeba
Picha: Tiksa Negeri/AFP/Getty Images

Mawaziri hao wanakutana wakati serikali zao zikilenga kurekebisha mahusiano kufuatia msuguano juu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka miwili katika jimbo la Tigray.

Soma pia:Blinken aelekea Afrika

Blinken kisha atakutana na Waziri Mkuu Abiy Ahmed na viongozi wa vikosi vya Tigray ambavyo vilikabiliana na serikali ya shirikisho katika vita vya jimbo hilo la kaskazini.

Baadae Blinken ataelekea katika taifa la Afrika Magharibi la Niger hapo kesho, ambalo limekuwa likipambana na ongezeko la uasi wa itikadi kali.