1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Blinken kukutana na Abbas baada ya ziara ya Israel

10 Januari 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken anatarajiwa kufanya mazungumzo hivi leo na rais wa mamlaka ya ndani ya Wapalestina, Mahmoud Abbas.

https://p.dw.com/p/4b3G9
Mzozo wa Mashariki ya Kati | Mkutano Antony Blinken na Mahmoud Abbas
Antiny Blinken akiwa na rais wa Mamlaka ya Wapalestina Mahmoud AbbasPicha: Evelyn Hockstein/REUTERS

Akiwa katika ziara ya nne Mashariki ya Kati tangu vita vilipoanza katika Ukanda wa Gaza, Blinken alikutana jana na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mjini Tel Aviv.

Blinken alisema Israel lazima iwache kuchukua hatua zinazohujumu uwezo wa Wapalestina kujitawala wenyewe, akisisitiza umuhimu wa kupiga hatua kuelekea suluhisho la mataifa mawili.

Soma pia:Blinken akutana na Rais wa Misri kujadili mizozo ya kikanda 

Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Marekani pia alisema mamlaka ya ndani ya Wapalestina ina jukumu la kufanya mageuzi ya ndani kuboresha utawala wake, masuala ambayo atayajadili na rais Abbas.