1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken aapa kumuunga mkono rais wa Niger aliyepinduliwa

Sylvia Mwehozi
29 Julai 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, ametangaza kumpa msaada wa dhati Rais wa Niger aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum.

https://p.dw.com/p/4UXDA
 Mohamed Bazoum
Rais wa Niger aliyepinduliwa Mohamed BazoumPicha: Ludovic Marin/AFP

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, ametangaza kumpa msaada wa dhati Rais wa Niger aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum.Jeshi na wananchi waunga mkono mapinduzi ya Niger

Blinken amewatahadharisha wanaomshikilia kiongozi huyo kuwa, msaada wa kifedha wa mamilioni ya dola kwa taifa hilo uko hatarini. Taarifa ya msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni wa Marekani Matt Miller imesema Blinken ametangaza kwa mara nyingine kuwa Marekani inamuunga mkono Bazoum wakati alipokuwa akikamilisha ziara yake katika mataifa kadhaa ya ukanda wa Pasifiki jana Ijumaa.

Matamshi ya Blinken yametolewa siku moja baada ya Jenerali Abdourahamane Tchiani kujitangaza kuwa kiongozi mpya wa mpito wa Niger baada ya mapinduzi ya kijeshi ya nchi hiyo yaliyotokea Jumatano wiki hii. Washington ilikuwa tayari imeonya kuwa inaweza kusitisha ushirikiano wa kiusalama na nchi hiyo.