1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken kuhudhuria mkutano wa usalama wa Munich

Sylvia Mwehozi
15 Februari 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ameanza ziara ya Ulaya, wakati wasiwasi ukizidi kuongezeka juu ya utawala wa Marekani.

https://p.dw.com/p/4cPf7
Antony Blinken
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony BlinkenPicha: Evelyn Hockstein/REUTERS

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ameanza ziara ya Ulaya, wakati wasiwasi ukizidi kuongezeka juu ya utawala wa Marekani. Blinken anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa usalama wa Munich, akiambatana na makamu wa rais Kamala Harris.

Kabla ya kufika mjini Munich, Blinken ataitembelea Albania, mshirika wa karibu wa Marekani ambayo imeiunga mkono Ukraine katika mapambano yake na Urusi. 

Ziara hiyo inafanyika wakati bunge nchini Marekani, likikwama kuidhinisha msaada kwa Ukraine. Rais wa zamani Donald Trump anashinikiza chama chake cha Republican kutoidhinisha msaada mpya wa kijeshi na kiuchumi ndani ya bunge ili kuisadia Ukraine.

Kuanzia kesho hadi Februari 18, maafisa wa jeshi, wataalamu wa ulinzi na wanasiasa kutoka kote ulimwenguni watakutana mjini Munich, kusini mwa Ujerumani kwa mkutano wa masuala ya usalama.