1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken aahidi uungaji mkono wa Marekani kwa Afghanistan

Saleh Mwanamilongo
15 Aprili 2021

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani,Antony Blinken ameahidi kuwa Marekani itaendelea kuwa na ushirikiano wa kudumu na Afghanistan.

https://p.dw.com/p/3s532
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani ,Antony Blinken (kushoto) na Abdullah Abdullah ,Mkuu wa baraza ya maridhiano ya kitaifa nchini Afghanistan, Kabul.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani ,Antony Blinken (kushoto) na Abdullah Abdullah ,Mkuu wa baraza ya maridhiano ya kitaifa nchini Afghanistan, Kabul.Picha: High Council for National Reconciliation Press Office/ REUTERS

Blinken ametoa ahadi hiyo wakati wa ziara yake ambayo haikutangazwa nchini Afghanistan. Kwenye ziara hiyo ya kushitukiza, Blinken amekutana na rai wa Afghanistan, Ashraf Ghani pamoja na maafisa wakuu wa Marekani mjini Kabul na kuwajulisha kuhusu ujumbe wa rais Biden uliotoloewa jana kuhusu kumalizika kwa vita vya muda mrefu vilivyoanza kufuatia mashambulizi ya Septemba 2001.

‘'Nilitaka kuonyesha kupitia ziara hii uungaji mkono unaondelea wa Marekani kwa Jamhuri ya kiislamu na raia wa Afghanistan'',alisema Blinken baada ya kukutana na rais Ghani.

‘'Ushirikano unabadilika, lakini ushirikiano huo ni wa kudumu'',aliendelea kusema.

Mwanzo wa ukarasa mpya ?

Kwenye mkutano tofauti na Mkuu wa Baraza la maridhiano ya Kitaifa, Abdullah Abdullah, waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani alisema kuwa huo ni mwanzo wa ukarasa mpya ambao umeandikwa kwa pamoja.

Ukraine Ukrainischer Präsident Selenskyj besucht Militär in Donbass
Picha: Ukrainian Presidential Press Off/AP/picture alliance

Wizara ya ulinzi ya Marekani, Pentagon, inao wanajeshi wapatao 2500 nchini Afghanistan, kutoka zaidi ya 100,000. Maelfu ya wanajeshi wengine wamefanya kazi chini ya kivuli cha Jumuiya ya Kujihami ya NATO yenye wanajeshi 9,600 ambao pia wataondoka kwa wakati mmoja.

Kabla ya kukutana na rais Ghani, Blinken alikwenda kwanza kwenye Ubalozi wa Marekani mjini Kabul, ambako aliwahutubia Wamarekani wengi wao wakiwa wanajeshi.

Amewaambia kwamba kazi ambayo wao na watangulizi wao waliifanya mnamo miaka 20 iliopita ni ya muhimu sana.

Kuondoka bila masharti, miezi minne baada ya muda ulioafikiwa na wapiganaji wa Taliban mwaka uliopita, kumekuja licha ya mkwamo wa mazungumzo ya amani baina ya wanamgambo na serikali. Kuondolewa huko kwa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan kunazusha wasiwasi kuhusu usalama wa nchi hiyo.

Kuondoka kwa wanajeshi hao kumezua huzuni ya raia wa nchi hiyo ambao wanaishi na woga wa mashambulizi ya anga na mauwaji ya wapiganaji wa taliban.

Mbunge Naheed Farid amesema kwamba hisia zake ni za kupoteza matumaini kufuatia hatua hiyo ya Marekani.

Vita visivyo kwisha Afghanistan

Afghanistan Heart | Artillerie-Training der Armee durch US-Army
Picha: DW/S. Tanha

Metra Mehran, mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake mjini Kabul, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani kunaweza kupoteza yote yaliofanyika miaka 20 iliopita na kuhatarisha usalama wa nchi hiyo.

Lakini Marekani imehisi kwamba baada ya miaka 20 na kupoteza wanajeshi wake 2,400 ni wakati sasa wakukomesha vita hivyo.

Jeshi la Marekani halijaendesha makabiliano na wapiganaji wa Taliban toka kutiwa saini mkataba wa amani wa mwaka uliopita. Aidha jeshi la Marekani linatoa msaada wa kijeshi kwa jeshi la anga la Afghanistan.

Watalibani wasusia mwito wa Uturuki

Baada ya mazungumzo ya simu na Biden siku ya Jumatano, rais Ghani alisema kuwa vikosi vya Afghanistan vina nguvu ya kuhakikisha usalama wa taifa.

Mapigano yameendelea nchini humo, licha ya miezi kadhaa ya mazungumzo huko Qatar baina ya Wataliban na serikali ya Afghanistan.

Uturuki ilitangaza wiki hii kuandaa mkutano wa kimataifa wa amani kwa matumaini ya kufikia makubaliano kuhusiana na kuleta amani Afghanistan, taifa ambalo limekumbwa na vita kwa karibu miaka 40. Lakini wanamgambo wa Taliban wamesema hawatohudhuria mkutano huo.