1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BLANTYRE:Mama Chirwa kuwania Urais Malawi

5 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFlu
Kamishna wa haki za binaadamu kwa Umoja wa Afrika Mama Vera Chirwa ametangaza leo hii kwamba atagombea Urais katika uchaguzi wa Rais uliopangwa kufanyika mwezi wa Mei nchini Malawi na kuwa mwanamke wa kwanza kuwania wadhifa huo nchini humo.

Mama Chirwa ameliambia shirika la habari la The Associated Press kwamba wanaume wamekuwa wakihodhi siasa za Malawi kwa muda mrefu mno na hiyo pengine ndio sababu kwa nini wanavurunda. Chirwa mwenye umri wa miaka 71 amesema anafikiri iwapo mwanamke atajitokeza ataweza kuboresha mambo mengi.

Orton hayati mume wa Chirwa aliakiasisi chama cha Malawi Congress na kutumika kama waziri wa sheria chini ya utawala wa Rais wa kwanza wa nchi hiyo Hastings Kamuzu Banda.Chirwa na mumuwe walipatikana na hatia ya uhaini hapo mwaka 1981 na kuhukumiwa kunyongwa kwa kuunda chama cha upinzani.

Hukumu hiyo iligeuzwa kifungo cha maisha na Banda alimpa msamaha Vera Chirwa baada ya mume wake kufariki gerezani.