1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BLANTYRE:Kesi ya uhaini ya Makamu wa rais wa Malawi yaanza tena

31 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCWU

Kesi ya Uhaini inayomkabili Makamu wa Rais wa Malawi Cassim Chilumpha ilianza tena hapo jana .Mwendesha mashtaka mkuu Wezi Kayira alifuta mashtaka yaliyomkabili mmoja wa washtakiwa Rashid Nembo kwasababu ya ukosefu wa ushahidi.

Bwana Chilumpha pamoja na Rashid Nembo na mfanyibiashara mashuhuri Yusuf Matumula walishtakiwa kwa madai ya kupanga kumuua Rais Bingu wa Mutharika kwa kutumia wauaji wa kukodisha kutoka Afrika Kusini.

Makamu wa Rais Cassim Chilumpha anakanusha madai hayo na kudai kuwa anateswa kwa kukataa kujiunga na Chama cha Democratic Progressive Party kilichoanzishwa na Rais Mutharika baada ya kukihama Chama tawala cha United Democratic Front.