1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BISSAU: Uchaguzi wa rais - Guinea Bissau

25 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEr6

Upigaji kura wa kumchagua rais mpya katika taifa la Afrika Magharibi la Guinea Bissau umemalizika.Duru ya pili ya uchaguzi,siku ya Jumapili,iliwapambanisha marais wawili wa zamani-mgombea wa chama tawala Malam Bacai Sanha na mgombea wa kujitegemea Joao Bernardo Vieira,ambae utawala wake wa mabavu ulikatizwa kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1999.Vieira alikimbilia Ureno,mkoloni wa zamani wa Guinea Bissau na alirejea nyumbani kutoka uhamishoni mwezi wa Aprili na alipokewa kwa shangwe kubwa.Uchaguzi wa jumapili umefanywa siku chache tu baada ya majengo ya serikali kushambuliwa.Polisi wawili waliuawa na wengi wengine walijeruhiwa katika mashambulio hayo.Matokeo ya uchaguzi yanatazamiwa kutangazwa katika kipindi cha wiki moja