1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden: Urusi kusitisha mkataba wa nyuklia ni kosa kubwa

22 Februari 2023

Rais wa Marekani, Joe Biden amesema Rais wa Urusi Vladimir Putin amefanya kosa kubwa kwa kusimamisha ushiriki wa nchi yake katika mkataba wa kudhibiti silaha za nyuklia baina ya mataifa hayo mawili.

https://p.dw.com/p/4NqoW
Warschau NATO-Treffen Bukarest 9
Picha: EVELYN HOCKSTEIN/REUTERS

Rais huyo wa Marekani ameyasema hayo akiwa Poland kutoa hakikisho la taifa lake kwa washirika wake wa Jumuia ya Kujihami ya NATO wa upande wa mashariki.

Biden amesema taifa lake litakuwa karibu yao katika kipindi hiki cha uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Mataifa mengi kama vile Bulgaria, Jamhuri ya Czech, Estonia, Hungary, Latvia, Lithuania, Poland, Romania na Slovakia yana mashaka kuwa huenda Rais Putin akachukua hatua za kijeshi dhidi yao endapo atafanikiwa katika vita vyake dhidi ya Ukraine.