1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMexico

Biden, Trudeau na Lopez kujadili uhamiaji nchini Mexico

9 Januari 2023

Mzozo wa kikanda juu ya uhamiaji na ulanguzi wa dawa za kulevya unatarajiwa kutawala mazungumzo kati ya Rais wa Marekani Joe Biden na mwenzake wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador leo viongozi hao wawili watakapokutana.

https://p.dw.com/p/4Ltli
Mexiko Zumpango | Joe Biden und Andres Manuel Lopez Obrador am Flughafen
Picha: Fernando Llano/AP Photo/picture alliance

Huku biashara na masuala ya mazingira yakiwa yanatarajiwa kujadiliwa katika mkutano huo utakaomjumuisha pia Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, Biden ameyapa kipau mbele masuala ya ongezeko la uhamiaji na ulanguzi wa madawa ya kulevya katika ziara yake hiyo ya kwanza nchini Mexico tangu achukue uongozi.

Alipokuwa njiani kuelekea Mexico kwa mkutano huo wa kilele uliopewa jina "Three Amigos" au mkutano wa kilele wa marafiki watatu, Biden alisimama kwa masaa kadhaa katika mji wa El Paso huko Texas, mji unaopakana na Mexico  na unaokabiliwa na tatizo hilo la uhamiaji.

Aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump aliwahi kutangaza mpango wa kujenga ukuta kwenye mpaka kati ya Mexico na Marekani.