1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden na Xi Jinping wakabiliana kwa njia ya simu

29 Julai 2022

Marais wa Joe Biden na Xi Jinping wapo katika kutafuta uwezekano wa kufanya mkutano wa ana kwa ana baada ya kutumia zaidi ya saa mbili kujadili hatma ya uhusiano wao tete pamoja na kuibuka tena mvutano kuhusu Taiwan.

https://p.dw.com/p/4EqOC
USA Joe Biden bei einem Telefongepräch mit Xi JinpinG
Picha: White House/ZUMAPRESS.com/picture alliance

Kwa mujibu wa afisa ambae alizungumza kwa masharti ya kutotajwa jila lake alisema akiwa na wasaidizi wake wakuu, akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani, Antony Blinken, Biden alipiga simu akiwa katika Ikulu ya Marekani. Katika kipindi ambacho Biden alikuwa makamo wa rais anaelezwa kutumia kipindi kirefu kwa China au Marekani kuzungumza na Xi Jinping kuhusu masuala mbalimabali kuhusu mataifa hayo, lakini tangu awe rais mwaka uliopita, hawajakutana.

Tangu kuzuka kwa janga la Covid-19, Xi aliwahi kutoka nje ya China Bara mara moja, kwenda Hong Kong. Hata hivyo ni rasmi amepewa mwaliko katika mkutano wa kundi la mataifa 20 tajiri na yanayoinukia kiuchumi G20 unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu nchini Indonesia, eneo ambalo linatoa sura muhimu ya uwezekano wa viongozi hao kukutana ana kwa ana.

Mazungumzo yalimazika kila upande kusalia na msimamo wake.

China Xi Jinping  bei einer Videokonferenz mit Joe Biden
Rais Xi Jinping wa China Picha: Huang Jingwen/Xinhua News Agency/picture alliance

Lakini kwa zingatio la mazungumzo haya ya Alhamis, na taarifa za upande wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Xi ameendelea kusimamia msimamo wa taifa lake kuhusu kisiawa cha Taiwan, kwamba ni shemu ya China na kwamba yeyote anaechezea na moto kwa uhakika utamuunguza. Kiongozi huyo ameongeza kwa kusema ni matumaini yake kuwa Marekani italitazama jambo hilo kwa macho mawili.

Na Ikulu ya Marekani imetoa maelezo yake kuhusu Taiwan, ikisema Biden amesitiza kuwa sera ya Marekani haijabadilika na kwamna taifa hilo linapinga vikali jitiahada binafsi za China za kufanyia mabadiliko hali ilivyo sasa au kuvuruga amani na utulivu katika eneo la Ujia wa Bahari wa Taiwan.

Karine Jean Pierre ni msemaji wa Ikulu ya Marekani anasema "Haya yalikuwa mazungumzo nyoofu. Wanamahusiano kwa miongo kadhaa. Hii ni simu ya tano rais amempigia Xi. Wanataka kuhakikisha kwamba wanaendeleza mazungumzo, waliweka wazi jambo hilo na ndivyo tulivyoshuhudia leo."

Ikulu ya Marekani imesema lengo la mawasiliano hayo ya simu ambayo yalianza saa mbili na nusu Asubuhi na kunalizika saa  nne na dakika 50 ni kusimamia tofauti zilizopo baina ya mataifa hayo na kufanya kazi pale ambapo kuna maslahi ya pamoja. Kwa kawaida China imekuwa ikiitupia lawama Marekani kutoka na kuzorota kwa mahusiano baina ya mataifa hayo mawili.

Soma zaidi: China yaishutumu Marekani kwa kuipaka tope

Awali Jumatanao, Msemaji wa Idara ya Usalama wa Taifa ya Marekani, John Kirby alisema ni muhimu kwa Biden na Xi kuweka msingi wa kuyajadili mara kwa mara mambo muhimu baina ya taifa hayo. Kwa mara ya mwisho Biden, kuzungumza na X ilikuwa mwezi Machi, kiopindi kifupi baada ya Urusi kuivamia Ukraine.

Chanzo: AP