1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden na Trump kukabiliana katika mdahalo wa kwanza 2024

27 Juni 2024

Wagombea wa urais nchini Marekani, Joe Biden na Donald Trump, watakabiliana siku ya Alhamisi katika mdahalo wa kwanza kati ya miwili kabla ya uchaguzi wa Novemba.

https://p.dw.com/p/4hbFD
Hii ni mara ya tatu kwa Biden na Trump kukutana kwenye jukwaa la mdahalo.
Hii ni mara ya tatu kwa Biden na Trump kukutana kwenye jukwaa la mdahalo.Picha: imago images

Hayo yanajiri huku wagombea hao wote wawili wakilenga kutumia mdahalo huo kuwavutia wapiga kura ambao bado hawajafanya maamuzi.

Hii ni mara ya tatu kwa Biden na Trump kukutana kwenye jukwaa la mdahalo.

Mwaka 2020, mdahalo baina ya wagombea hao uligubikwa na janga la UVIKO-19, wakati huu leo ukitarajiwa kuzingirwa na masuala mashaka kuanzia ya umri, afya ya akili na uwezo wa kudhibiti hasira.

Biden, mgombea wa chama cha Democrat ana umri wa miaka 81, huku mtangulizi wake Trump wa Republican akiwa na miaka 78.

Kwa ujumla, hawa ni wagombea wenye umri mkubwa zaidi kuwahi kuwania urais.