1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden na Kishida kufanya mazungumzo juu ya usalama

13 Januari 2023

Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida wanatarajiwa hivi leo kufanya mazungumzo ya kina katika Ikulu ya White House.

https://p.dw.com/p/4M7Lz
Japan USA | Fumio Kishida und Joe Biden
Picha: AFP

Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida wanatarajiwa hivi leo kufanya mazungumzo ya kina katika Ikulu ya White House wakati Japan ikilenga kujenga uhusiano wa usalama na washirika wake kutokana na kuongezeka kwa wasiwasi wa uchochezi wa China na hatua ya kijeshi ya Korea Kaskazini.

Serikali hizo mbili pia ziko tayari kufikia makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wa Marekani na Japan kuhusu anga za mbali katika hafla ya utiaji saini na Waziri wa Mambo ya Kigeni Antony Blinken na mwenzake wa Japan Hayashi Yoshimasa. Mikutano hiyo ya White House na makao makuu ya NASA mjini Washington inafikisha kilele ziara ya wiki nzima ya Kishida iliyomfikisha katika miji mataifa matano ya Ulaya na Amerika Kaskazini kwa mazungumzo kuhusu juhudi zake za kuimarisha usalama wa Japan.