1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden kutofunguliwa mashitaka kwa nyaraka za siri

9 Februari 2024

Wizara ya Sheria ya Marekani imesema Rais Joe Biden hatafunguliwa mashitaka ya jinai kutokana na kuzihifadhi kwa makusudi nyaraka za siri baada ya kuhudumu kama makamu wa rais.

https://p.dw.com/p/4cDA4
Joe Biden
Rais Joe Biden wa Marekani ameepukana na uwezekano wa kushitakiwa kwa kukutwa na nyaraka za siri za serikali.Picha: Evan Vucci/AP/picture alliance

Mwanasheria maalumu aliyechunguza madai hayo Robert Hur amesema amechukua uamuzi huo wa kutomshitaki kwa sababu Biden alionyesha ushirikiano wakati wa uchunguzi wa tuhuma hizo.

Biden ameeleza kuridhishwa na hatua hiyo ya Hur ya kuhitimisha uchunguzi huo bila ya kumfungulia mashitaka.

Soma zaidi: Blinken aondoka Mashariki ya Kati bila mafanikio

Hata hivyo, ripoti ya mwanasheria huyo imeibua mashaka juu ya kumbukumbu ya kiongozi huyo ikieelezea kuwa ni mbaya mno kiasi cha kusahau hata mafanikio yake binafsi, hali inayoweza kudhoofisha zaidi imani ya raia kwa Biden anayedai bado anaweza kuongoza serikali.