1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden atangaza dola bilioni 1 kwa kukabiliana na joto

20 Aprili 2023

Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza ufadhili mwingine wa Marekani wa kimazingira wenye thamani ya dola bilioni moja.

https://p.dw.com/p/4QMmB
USA, Accokeek | Präsident Joe Biden
Picha: Patrick Semansky/AP/picture alliance

Haya ni wakati wa mkutano wa mtandaoni na viongozi kutoka mataifa makubwa kiviwanda duniani, uliofanyika hii leo kuratibu juhudi za kuzuwia ongezeko la joto la dunia. Mkutano huo wa Jukwa la Chumi Kubwa kuhusu Nishati na Tabianchi, ambao ikulu ya White House imesema ulihudhuriwa na maafisa, akiwemo mjumbe wa masuala ya tabianchi wa China, Xie Zhenhua na rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva, ulikuwa wa nne kuitishwa na Biden tangu alipoingia madarakani mwaka 2021. Biden ametangaza mchango huo wa dola bilioni moja kwa Taasisi ya Green Climate Fund, ambayo inafadhili juhudi za mataifa tajiri kusaidia chumi zinazokuwa kuhamia kwenye nishati safi zaidi, na kujenga miundombinu thabiti kwa tabianchi.