1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden akabiliwa na shinikizo kuhusu kampeni yake ya urais

Sylvia Mwehozi
3 Julai 2024

Rais wa Marekani Joe Biden anakabiliwa na shinikizo zaidi la kumtaka ajiengue katika kinyang'anyiro cha kuwania urais katika uchaguzi wa mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4hoBA
U.S. President Joe Bidens Äußerungen auf einer Wahlkampfveranstaltung nach der CNN-Präsidentschaftsdebatte
Rais wa Marekani Joe BidenPicha: Kyle Mazza/NurPhoto/IMAGO IMAGES

Baadhi ya wanachama wa chama cha Democrats, wamezusha kwa mara nyingine wasiwasi wao kuhusu jaribio la Biden la kuwania urais huku mmoja wao akimtaka kwa uwazi kuachia ngazi.

Miito ya kumtaka Biden kujiuzulu imeongezeka haswa baada ya kiongozi huyo kuboronga wakati wa mdahalo wa kwanza na mpinzani wake Donald Trump wa Republican.

Soma pia:Biden aboronga wakati Trump akitoa uongo mdahalo wa urais 

Baadhi ya wafadhili wameeleza wasiwasi wao kwamba hana uwezo wa kumshinda Trump katika uchaguzi wa Novemba.

Duru zinasema wanachama wapatao 25 wa Democrats katika Baraza la Wawakilishi wanajiandaa kuwasilisha ombi rasmi la Biden kujiengua.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni huko Virginia, Biden alikiri kwamba hakufanya vyema wakati wa mdahalo kutokana na uchovu wa safari alizofanya kabla.