1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden ahofia kusambaa kwa machafuko ya Mashariki ya Kati

2 Agosti 2024

Rais wa Marekani Joe Biden anasema ana wasiwasi mkubwa wa kuenea kwa machafuko ya Mashariki ya Kati.

https://p.dw.com/p/4j1wk
Rais wa Marekani Joe Biden
Rais Joe Biden akizungumza katika hafla ya kuadhimisha Miaka 60 ya Sheria ya Haki za Kiraia, Julai 29, Texas huko Marekani.Picha: Eric Gay/AP Photo/picture alliance

Na kuongeza kwamba kuuwawa kwa kiongozi mkuu wa Hamas nchini Iran, hakujasaidia juhudi za mazungumzo ya kusitishwa kwa vita vya Israel dhidi ya Hamas Biden amesema hapo jana alizungumza na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na kwamba kwa sasa wana msingi wa usitishwaji wa mapigano na amemtakawaziri mkuu huyo kuanza utekelezaji wake sasa. Waziri wa mambo ya kigeniwa Marekani Antony Blinken ni miongoni mwa sauti za kimataifa zinazoongezeka kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano katika siku za hivi karibuni, akisema hiyo ndiyo njia ya pekee ya kuanza kuuvunja mzunguko wa machafuko na mateso.