1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaCanada

Biden afanya ziara nchini Canada

24 Machi 2023

Rais Joe Biden wa Marekani amewasili nchini Canada jana Alhamisi kwa mazungumzo na waziri mkuu Justin Trudeau.

https://p.dw.com/p/4PA01
Kanada, Ottawa | Joe Biden trifft Justin Trudeau
Picha: Blair Gable/REUTERS

Mazungumzo kati ya viongozi hao wawili yatakayojikita katika changamoto kubwa ulimwenguni kuanzia vita nchini Ukraine, mabadiliko ya tabianchi, biashara, idadi kubwa ya wahamiaji na kuongezeka kwa uthabiti wa China.

Kwenye ziara hiyo wakuu hao wamefikia makubaliano yanayolenga kuwazuia waomba hifadhi kuingia kwenye mataifa hayo kwa kupitia njia zisizo rasmi, ingawa baadhi ya masuala yanatarajiwa kujadiliwa kwa kina watakapokutana kwa mazungumzo, vimesema vyanzo kutoka pande hizo mbili vilipozungumza na shirika la habari la Reuters.

Soma pia: Biden, Trudeau wakuza mahusiano ya Marekani na Canada

Pande zote mbili zinayachukulia mazungumzo hayo katika mji mkuu Ottawa kama fursa ya kupanga mikakati ya siku za usoni.