1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden afanya mazungumzo na mjane na binti wa Navalny

23 Februari 2024

Rais wa Marekani Joe Biden hapo jana Alhamisi alifanya mazungumzo ya faragha na mjane pamoja na bintiye marehemu Alexei Navalny mjini California.

https://p.dw.com/p/4cn3K
San Francisco| Rais Joe Biden akiwa na mke na binti wa Alexei Navalny
Rais Joe Biden akiwa na mke na binti wa Alexei Navalny, San Francisco.Picha: White House/ZUMA Press/dpa/picture alliance

Mkutano huo umefanyika huku utawala wa Biden ukitangaza vikwazo vipya dhidi ya Urusi kufuatia kifo cha kiongozi huyo wa upinzani nchini urusi.

"inashangaza jinsi mke na binti yake wanavyoiga hilo. Tutakuwa tukitangaza vikwazo dhidi ya Putin, ambaye alihusika na kifo chake, kesho. Lakini jambo moja ambalo wameliweka wazi kwangu ni kwamba, Yulia ataendelea na pambano," alisema Biden.

Timu ya Navalny inasema mkosoaji huyo mkubwa wa Rais Vladimir Putin, aliyekuwa na umri wa miaka 47, aliuawa.

Soma pia: Mjane wa Navalny aahidi kuendeleza kazi yake

Mkutano wa San Francisco ulijiri wakati Ikulu ya Marekani ikiunga mkono juhudi za mamake Navalny za kutaka kukabidhiwa mwili wa mwanawe, jambo ambalo mafias awa Urusi wamekataa, siku kadhaa tangu alipokufa gerezani.

Mama wa Navalny amesema ameuona mwili wa mwanawe na kwamba anapinga shinikizo kubwa la mamlaka kumtaka akubali mwanawe  azikwe kisiri bila umma kushuhudia.