1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden aendelea kushinikizwa asiwanie

5 Julai 2024

Rais Joe Biden anaendelea kukabiliwa na wito wa kujitowa kwenye kinyang'anyiro cha urais na kumpisha mgombea mwengine wa chama chake kupambana na Donald Trump kwenye uchaguzi wa Novemba mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4htE1
Rais Joe Biden wa Marekani.
Rais Joe Biden wa Marekani.Picha: Evan Vucci/AP/dpa/picture alliance

Magavana na wabunge kadhaa wa chama chake wanangoja mahojiano ya Biden  na kituo cha utangazaji cha ABC baadaye leo, kuamua ikiwa waendelee kumuunga mkono ama la.

Shinikizo hili la sasa linatokana na kushindwa vibaya kwa Biden kwenye mdahalo wake na Trump wiki iliyopita.

Soma zaidi: Biden akataa kujitowa kinyang'anyiro cha urais Marekani

Makamu wake, Kamala Harris, anaangaliwa na wengi kwamba ndiye atakayewania urais, endapo Biden atalazimika kujitowa.

Hata hivyo, Ikulu ya White House imesema kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 81 hana mpango wa kuchukuwa hatua hiyo.