1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden aahidi msaada kwa Ireland Kaskazini

12 Aprili 2023

Rais wa Marekani Joe Biden amesema neema kwa Ireland Kaskazini ndio imeanza na ameahidi msaada mkubwa wa Marekani kwa eneo hilo lililo sehemu ya Uingereza.

https://p.dw.com/p/4Pxzg
Rais Joe Biden akiwa mjini Belfast
Rais Joe Biden wa Marekani akitoa hotuba katika Chuo Kikuu cha Ulster mjini Belfast wakati wa ziara yake Ireland Kaskazini.Picha: Patrick Semansky/AP Photo/picture alliance

Biden ameyasema hayo wakati wa kumbukumbu ya miaka 25 tangu kutiwa saini makubaliano ya kuleta amani maarufu kwa jina la Ijumaa Kuu.

Katika hotuba yake katika chuo kikuu cha Ulster, Biden amesemamkataba huo uliosimamiwa na Marekani ulileta amani katika eneo hilo la Uingereza lakini mgogoro mpya wa kisiasa hivi karibuni unatishia uthabiti wake.

Biden ameongeza kuwa katika siasa, haijalishi kinachotenganisha, iwapo watu wanakuwa makini zaidi, kuna sehemu ambazo zinaweza kuwaunganisha.