Biden aahidi dola milioni 600 kwa mradi wa reli Afrika
5 Desemba 2024Rais huyo wa Marekani amewaambia viongozi wa Afrika kwamba bara hilo limeachwa nyuma kwa muda mrefu.
Biden pia alifanya ziara kwenye mradi wa reli wa Lobito na kuutaja kama uwekezaji mkubwa zaidi wa treni wa Marekani nje ya nchi hiyo.
Soma pia:Biden amsamehe mwanawe Hunter mashtaka ya jinai
Viongozi wa Afrika waliokutana na Biden hapo jana, walisema reli hiyo inazipa nchi zao njia ya haraka zaidi ya kusafirisha madini na bidhaa, pamoja na kuyafikia kwa urahisi masoko ya Magharibi.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi, ambaye nchi yake ina zaidi ya asilimia 70 ya madini ya kobalti duniani, amesema mradi huo umeongeza matumaini kwa mataifa yao na kanda nzima na kuongeza kuwa hatua hiyo ni msukumo wa mabadiliko ya kiuchumi na kijamii kwa mamilioni ya watu wao.