1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bibi Bush ziarani Rwanda

14 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEuS

Kigali:

Mke wa Rais wa Marekani, Bibi Laura Bush, leo ameweka shada la maua kwenye makaburi ya pamoja yaliyoko kwenye jengo la kumbukumbu ya mauaji ya halaiki mjini Kigali, Rwanda. Bibi Bush, akiandamana na Binti wake Jenna, mke wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Cherie Blair na Mama Jeanette Kagame, ameweka shada hilo la maua katika Jengo la Makumbusho la Gisozi ambako Wahanga 800,000 wameuawa wakati wa mauaji ya halaiki nchini Rwanda mwaka 1998. Bibi Bush, ambaye amewasili Kigali akitokea Tanzania, amesema kuwa Wamarekani wako nyuma ya Wanyaruanda wakati wanajitahidi kutengeneza siku nzuri za usoni. Marekani itahakikisha kuona kuwa kile kilichotokea wakati ule hakitokei tena. Bibi Blair naye amesema kuwa ni jambo la kusikitisha sana kuona kuwa wakati mauaji hayo yalipotokea ulimwengu ulitumbua macho. Bibi Bush, baada ya kuweka shada la maua, amehudhuria mkutano wa Wanawake na Demokrasia, atatembelea miradi ya elimu na atakutana na Rais Paul Kagame.