Beyrouth: malaki wanaandamana kujua ukweli wa kifo cha hariri
14 Machi 2005Matangazo
Zaidi ya waandamanaji laki nane wamekusanyika katika uwanja wa "Mashujaa" mjini Beyrouth hii leo,wakijibu mwito wa vyama vya upinzani.Wananchi zaidi na zaidi wanaendelea kumiminika kutoka sehemu mbali mbali za Libnan.Dhamana mmoja wa baraza la mjui la Beyrouth Mounib Nasserdine anasema idadi ya waandamanaji wa leo imepundukia mara mbili na nusu wale waliokusanyika jumanne iliyopita katika uwanja wa Riad Solh mjini Beyrouth.Maandamano ya leo yameitishwa na upande wa upinzani kudai utafiti wa kina ufanywe kujua nani walikua nyuma ya kuuliwa waziri mkuu wa zamani Rafik Hariri February 14 iliyopita.