1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Mkutano wa kilele wa viongozi wa CDU,CSU,na FDP

1 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEfU

Viongozi wa vyama vya CDU,CSU na FDP wako mjini Berlin kwa ajili ya mkutano wao wa kilele wa kuandaa misingi ya serikali yao ya mseto ambayo huenda wakaiunda baada ya uchaguzi mkuu wa septemba 18.

Mtetezi wa ukansela wa vyama vya CDU na CSU Angela Merkel amesema mazungumzo hayo hayotokuwa ni mashauriano ya kabla ya uchaguzi lakini yatahusu tu juu ya mambo muhimu ambayo vyama hivyo vinakubaliana nayo.