1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin:Bundesrat limeidhinisha kujiungwa kwa Romania na Bulgaria, umoja wa Ulaya.

24 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCph

Baraza la mabunge ya mikoa ya Ujerumani-BUNDESRAT- limeidhinisha kujiunga kwa Rumania na Bulgaria na Umoja wa Ulaya.

Hatua hiyo inaondoa kikwazo cha mwisho na kufungua njia ya nchi hizo kuwa wanachama wa 26 na 27 kuanzia Januari mosi mwaka ujao.

Uamuzi huo unafuatia hatua sawa na hiyo iliochukuliwa na bunge la Ujerumani-BUNDESTAG- katika kura iliopigwa mwezi uliopita, na sasa maamuzi hayo yataidhinishwa na rais Horst Koehler.

Ujerumani na Denmark ni wanachama wa mwisho miongoni mwa 25 katika Umoja wa Ulaya, kuidhinisha kukubali rasmi uanachama wa Rumania na Bulgaria, kutokana na uamuzi wa halmashauri kuu ya umoja huo mwezi Septemba.