1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ukraine inahitaji msaada kuingia Umoja wa Ulaya

10 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFYI

Rais Viktor Yushchenko wa Ukraine amekamilisha ziara yake ya siku mbili mjini Berlin,akiwa miongoni mwa viongozi wachache wa kigeni kulihotubia bunge la Ujerumani,Bundestag.Rais Yushchenko aliitumia fursa hiyo kueleza kuwa anahitaji kuungwa mkono kutekeleza lengo lake la kuiongoza Ukraine kuingia Umoja wa Ulaya.Amesema Ukraine inahitaji msaada zaidi wa kigeni, ikijitahidi kuleta mageuzi ili iwe nchi ya kisasa yenye demokrasia,barani Ulaya.Hapo awali Yushchenko alikutana na Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani.Schroeder amekataa kupanga tarehe maalum ya kuipokea Ukraine kama mwanachama katika Umoja wa Ulaya,akisema huo ni uamuzi unaopitishwa na Halmashauri ya Ulaya.