1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ujerumani yakubali katiba ya Umoja wa Ulaya .

12 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFEN

Bunge la Ujerumani leo linatarajiwa kuidhinisha katiba ya Umoja wa Ulaya kwa theluthi mbili za kura za wabunge.

Hatahivyo wabunge wa vyama vya upinzani takriban 25 wanatarajiwa kuipinga katiba hiyo.

Katiba hiyo itaweza kutumika katika nchi zote za Umoja wa Ulaya ikiwa kama nchi zote zitaipitisha.

Ujerumani inaharakisha zoezi la kuipitisha katiba hiyo ili kutoa ishara nzuri kwa watu wa Ufaransa wanaotarajiwa kuipigia kura katiba hiyo.

Kansela wa Ujerumani bwana Gerhard Schröder leo anatazamiwa kutoa tamko la

kuitetea katiba hiyo ya Umoja wa Ulaya.

.