1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. SPD na CDU wana matumaini ya kuunda serikali ya mseto.

29 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEWe

Kansela wa Ujerumani Gerhard Schröder amesema kuwa anaimani chama chake cha Social Democrats kinaweza kuunda serikali imara ya mseto na chama cha mpizani wake Angela Merkel cha Christian Democrats.

Schröder alikuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya duru ya pili ya mazungumzo ya mwanzo , majadiliano yenye lengo la kusafisha njia kwa mazungumzo ya kuunda muungano.

Mwenyekiti wa chama cha SPD Franz Müntefering amesema kuwa pande hizo mbili zimekubaliana kukutana tena katika muda wa wiki moja.

Hakuna upande ulioeleza hatua gani zimepigwa katika mkutano wao, ambao ulitarajiwa kulenga katika masuala muhimu ya sera.

Bwana Schröder pamoja na Bibi Merkel wanadai kuwa na uhalali wa kuunda serikali ya kuiongoza nchi hiyo kufuatia uchaguzi uliofanyika mwezi huu ambao haukutoa mshindi kamili.