1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin: Siku moja tuu kabla ya mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya ...

11 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFt7
mjini Brussels,hatima ya katiba mpya ya umoja huo bado si dhahiri.Waziri mkuu wa Luxembourg Jean Claude Juncker ameonya kishindo kinachoweza kutokea pindi makubaliano yakishindikana mjini Brussels.Akihojiwa na gazeti la Berliner Zeitung waziri mkuu wa Luxembourg,Jean Claude Juncker amesema huenda waasisi wa umoja wa ulaya wakaamua kufuata njia yao wenyewe.Kabla ya hapo rais wa Poland Aleksander Kwasniewski aliiambia BBC atatumia kura ya turufu kuipinga katiba mpya ikiwa madai ya nchi yake hayatazingatiwa.Poland sawa na Hispania zinashikilia ztiendelee kuwa na sauti 27 dhidi ya 29 za madola yenye wakaazi wengi,Ujeruimani,Ufaransa,na Uengereza,kama ilivyotajwa ndani ya makubaliano ya Nice.Rais Alexander Kwasniewski anatazamiwa kuwasili mjini Berlin baadae hii leo na kuzungumza na kansela Gerhard Schröder.