1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Mkutano mkuu wa FDP kabla ya uchaguzi

12 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEc5

Chama cha kiliberali cha Ujerumani FDP kimekuwa na mkutano wake mkuu wa mwisho mjini Berlin,kabla ya uchaguzi mkuu wa wiki ijayo.Uchunguzi wa maoni uliyofanywa hivi karibuni,umeonyesha kuwa muungano wa FDP na wahafidhina,huenda ukakosa kupata uwingi unaohitajiwa bungeni,ili kuweza kuing’oa serikali ya mseto ya SPD na chama cha Kijani,inayoongozwa na Kansela Gerhard Schroeder.