1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Mfrakano ndani ya SPD watishia kuundwa serikali ya mseto

1 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEN0

Mfarakano ndani ya chama cha Social Demokrat SPD nchini Ujerumani umezidi kuwa mkubwa wakati chama hicho kikiingia katika dure ya nne ya mazungumzo na wahafidhina juu ya kuunda serikali ya mseto ya muungano mkuu nchini.

Kiongozi wa SPD Franz Münteferring ametangaza kwamba anajiuzulu kama mwenyekiti wa chama.Münteferring alikuwa atumike kama makamo kansela na waziri wa kazi katika serikali ya muungano mkuu na wahafidhina lakini hivi sasa amesema hana hakika iwapo atachukuwa nyadhifa hizo.Uamuzi wake wa ghafla unakuja baada ya chama cha SPD kupuuza kupinga kwake kuchaguliwa kwa kijana mfuasi wa sera za mrengo wa shoto kuwa katibu mkuu wa chama hicho.

Iwapo Münteffering atajitowa kwenye serikali mpya kunaweza kuleta taathira kubwa pengine hata kusababisa kuvunjika kwa mazungumzo ya kuunda serikali hiyo ya mseto na kufanyika kwa uchaguzi mpya iwapo wahafidhina wataona kwamba hawawezi tena kuendelea na mazungumzo ya kuunda serikali na SPD.