1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Merkel ataka kuzuiliwa kwa Uturuki kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya

27 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEhL

Kiongozi wa upinzani nchini Ujerumani Angela Merkel amewataka viongozi wa kihafidhina barani Ulaya kuungana naye katika kutaka kuipatia Uturuki ushirikiano wa upendeleo maalum ambao hautoifanya nchi hiyo kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Katika baruwa kwa viongozi wa Umoja wa Ulaya Merkel amesema kuingiza Uturuki kwenye umoja huo kutakuwa mzigo mkubwa kisiasa,kiuchumi na kijamii kwa Umoja wa Ulaya. Ameongeza kusema kwamba pia kutahatarisha mchakato wa maingiliano barani Ulaya.

Merkel pia ametaja kwamba kukataa kwa Uturuki kuitambua Cyprus kuwa ni kikwazo kwa uwanachama wa nchi hiyo kwa Umoja wa Ulaya.